Wednesday, 23 December 2015

PUMZIKA KWA AMANI (R.I.P) MLAWILA "LAWI" MGALULA FUNDIKIRA

Usiku wa tarehe 18 Disemba 2015, Jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni ilipata msiba mkubwa wa kijana Mlawila "Lawi" Mgalula Fundikira aqmbaye ni mtoto wa mwanajumuiya Mgalula Fundikira ambaye alikuwa katika uangalizi maalum wa kitabibu (ICU) kwa takriban juma moja katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kutokana na majeraha ya ajali. Makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni ndugu Mkala Fundikira, ambaye pia ni baba mdogo wa marehemu Lawi alitoa taarifa ya msiba huo kwa masikitiko makubwa ambapo mipango ya mazishi ilifanyika nyumbani kwa baba wa marehemu na mazishi yalifanyika katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam siku ya jumapili tarehe 19 Disemba, 2015.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya: Mkala Fundikira (kulia) akiwa pamoja na Wanajumuiya 

Baada ya kukamilisha shughuli za msiba, Mwanajumuiya Mgalula Fundikira alitoa salamu za shukrani wa wote walioshiriki msiba wa kijana wake aliandika haya: - 
"To my dear family and friends, My son Mlawila "Lawi" has finally been laid to rest and i am coming to accent however slowly and painfully that he is now in a better place, No words can ever express the way you all have made me feel during this most trying and difficult period in my life, I convey my utmost sincere gratitudes and appreciation for all the love, support and solidarity you have shared with my us and still do, On behalf of Mama Lawi, Nyanzala, Oliver and the rest of the Fundikira family, I can simply say Thank you all, Please keep on staying as amazing as you all have been, Much love and respect to all of you, Rest in Peace my son."

Pumzika kwa Amani (R.I.P) Mlawila "Lawi" Mgalula Fundikira.

No comments:

Post a Comment