Jumuiya ya Marafiki wa Kiondoni inazidi kupata wanachama wapya. Tarehe 19 Disemba, 2015
Mwanajumuiya mpya alijiunga rasmi katika Jumuiya hiyo, BI. Anna Mwengele
(pichani chini) akizungumzia namna alivyoifahamu Jumuiya alieleza kuwa mwanzoni
alidhani ni “group” tu la kuchati mtandaoni, lakini baada ya kukutana na
Wanajumuiya na kupata taarifa zote kuhusu Jumuiya, hakutaka kusubiri hata
kidogo na badala yake alifuata taratibu zote za kujiunga na Jumuiya na amekuwa
Mwanachama wa 41.
![]() |
| Anna Mwengele - Jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni |
Akimkaribisha rasmi
katika Jumuiya, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Marfiki wa Kinondoni, ndugu Ivan
Minja alimuasa bi Anna Mwengele kushiriki kikamilifu katika masuala yote ya
Jumuiya na pia kutoa maoni, mawazo pamoja na kutumia kipaji chake pamoja na
fursa mbalimbali katika kuyafikia malengo ya Jumuiya.
Akizungumza baada ya kukaribishwa rasmi kwenye Jumuiya, Bi. Anna alieleza furaha yake kuwa sehemu ya Jumuiya muhimu kwa maendeleo ya Wanakinondoni na ameridhishwa na namna Wanajumuiya wanavyojitolea katika masuala mbalimbali ya kijamii. Vilevile amewasisitiza Wanajumuiya wote uendeleza upendo na ushirikiano alioukuta na hiyo ndio iwe falsafa ya wote katika kuyafikia malengo ya Jumuiya.

No comments:
Post a Comment