Thursday, 24 December 2015

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA WIKI YA 52 YA MWAKA 2015 KWA JUMUIYA YA MARAFIKI WA KINONDONI

Wiki ya 52 ya mwaka 2015 imekuwa ya matukio mbalimbali kwa wanachama wa Jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni, katika wiki hii wanachama wawili wa Jumuiya wamesherehekea siku zao za kuzaliwa. Wanachama hao Bi. Remina Omary na Bi. Anna Mwengele wote wamezaliwa siku moja, yaani tarehe 22 mwezi Disemba.

Add caption
Kama ilivyo ada, Wanajumuiya hawakukosa katika kuwapongeza wanachama wenzao hao katika siku hiyo. Tirika na picha mbalimbali za tukio hilo hapa chini.
Remina Omari (katikati) akiwa pamoja na Abdul Kazembe (kushoto) na Mkala Fundikira (kulia)


Keki nazo zilikuwepo
Selfie ilihusika pia
 Tukio lingine ni ajali aliyopata mwenyekiti wa Jumuiya ndugu Yahya Poli iliyosababishwa na bodaboda. Wanajumuiya wamemtumia salamu za pole Mwenyekiti wao na kumuombea apone haraka ili aendelee na majumukumu yake ya kuijenga Jumuiya.
Sehemu ya jeraha alilopata Mwenyekiti baada ya matibabu
Mwanajumuiya, Esther Shayo naye wiki hii alizawadiwa tuzo ya mfanyakazi bora wa mwaka 2015 kwa wafanyakazi wa kampuni ya Porter Noveli. Wanajumuiya wanampongeza dada Esther kwa tuzo hiyo na wamemkumbusha kuwa tuzo hiyo ni changamoto y kuongeza bidii zaidi kazini. Vilevile wanajumuiya walishauri uongozi wa Jumuiya kuangalia uwezekano wa kuwa tuzo mbalimbali za mwaka kwa wanachama wake na ikiwezekana iwe ni kuanzia mwaka 2016.


Tuzo ya mfanyakazi Bora - 2015

Makamu Mwenyekiti MKala Fundikira (mbele) akiwa na nfanyakazi bora Esther Shayo
Katika kumalizia wiki hii pia Wanajumuiya watasherehekea sikukuu za kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambayo inasherehekewa tarehe 12 Rabi Al-Awaal 1437 A.H. sawa na tarehe 24 Disemba, 2015



Vilevile sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambayo husherehekewa tarehe 25 Disemba ya kila mwaka.


Jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni inawatakia wanachama wake na watu wote duniani heri ya sikukuu za Maulid na Krismasi na pia inawaasa kuzisherehekea siku hizo kwa kutenda matendo ya huruma nay a mpendezayo Mungu. 

No comments:

Post a Comment