Jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni, ni
umoja wa hiyari ulioanzishwa na wanajumuiya ambao wamezaliwa, wameishi au bado
wanaishi katika wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Ujirani mwema pamoja na upendo miongoni
mwa Wanajumuiya hao wakiwa wakaazi wa Kinondoni ndiyo iliyokuwa chachu ya kuleta ushirikiano mkubwa uliofananishwa na udugu baina yao. Harakati za kuanzisha Jumuiya zilianzia katika mitandao ya kijamii hususan katika mtandao wa Facebook ambapo zaidi ya Wanakinondoni 3000 waliotapakaa katika maeneo mbalimbali duniani wamekuwa wakiwasiliana na kupashana haabari na kumbukumbu. Hatimaye, tarehe 14 Juni, 2015 kikao cha kwanza kilifanyika katika ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni na kuwakutanisha Wanakinondoni na kujadili mustakbali wa Jumuiya yao chini ya uratibu wa Mwanakinondoni Ivan Minja.
![]() | |||
| Baadhi ya Wanakinondoni walipokutana katika vikao vya awali vyaa kuunda Jumuiya |
Hivyo basi, katika kuthamini mahusiano hayo,
Wanajumuiya kwa kauli moja, wakaanzisha Jumuiya hii kwa kuzingatia haja na
umuhimu wa kushirikiana kwa dhati katika masuala mbalimbali ya
kijamii na kuchangia maendeleo ya Mwanajumuiya mmoja mmoja, Wanajumuiya wote kupitia miradi ya Jumuiya
na Taifa kwa ujumla katika kuyafikia Malengo ya Jumuiya.
![]() |
| Baadhi ya Wanajumuiya katika picha ya pamoja baada ya kikao |
Katika kuipa nguvu Jumuiya, wanachama waliamua kuandaa Katiba na hatimaye kuteua uongozi wa muda ambao ungewezesha kukamilika kwa baadhi ya masuala kabla ya usajili rasmi wa Jumuiya katika mamlaka za nchi. Uchaguzi ulifanyika na viongozi wa muda waliochaguliwa ni Yahya Poli (Mwenyekiti), Mkala Fundikira, (Makamu Mwenyekiti), Suzana Samson (Katibu Mkuu), Ivan Minja (Katibu Msaidizi), Ismail Kagambo (Mweka Hazina), Flora Samwel (Mweka Hazina Msaidizi), Adam Bush, Juliana Kitundu, Mahmoud Kamus na Abdul Kazembe (wajumbe wa Kamati ya Utendaji).
![]() |
| Picha ya pamoja ya viongozi wa muda: Kutoka kushoto (waliokaa) Flora Samwel, Suzana Samson, Yahya Poli, Mkala Fundikira, Juliana Kitundu. Waliosimama; Abdul Kazembe, Mahmoud Kamus na Adam S. Bush |
Baada ya kukamilisha hatua za kuanzisha (setting-up) rasmi jumuiya hatimaye tarehe 14 Oktoba, 2015 ulifanyika Mkutano Mkuu wa kwanza wa Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni ambapo waliteuliwa; Yahya Poli (Mwenyekiti), Mkala Fundikira, (Makamu Mwenyekiti),
Ivan Minja (Katibu Mkuu), Suzana Samson (Katibu Msaidizi), Nancy Shemndolwa (Mweka Hazina), Ismail
Kagambo (Mweka Hazina Msaidizi), Adam Bush,
Juliana Kitundu na Halmat Yusuph (wajumbe wa Kamati ya
Utendaji), Moses Mahenge, Annda Nganda na Henry Maseko (Kamati ya Uchumi Mipango na Maendeleo.
![]() |
| Viongozi wa Jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni (2015 - 2018) katika picha ya pamoja na Wanajumuiya baada ya uchaguzi. |
Karibu katika Jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni.







No comments:
Post a Comment