Mwanachama wa Jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni ndugu Sebastian Kazimoto Ritte alipatwa na msiba wa kaka yake maarehemu Apolito Ritte (pichani chini)ambaye amefariki majira ya saa 6 usiku tarehe 5 Disemba, 2015 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Mwanajumuiya Sebastian (maarufu Seba) amewasili akitokea Marekani kwa ajili ya kushiriki mazishi ya kaka yake kufanyika leo mchana katika makaburi ya Kinondoni Dares Salaam.
![]() |
| Marehemu Apolito Anthony Kazimoto Ritte |
Shughuli za mazishi zilitanguliwa na misa/ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwao maeneo ya Kinondoni B, mtaa wa Isere maarufu kama chemchem ambako pia marehemu alikuwa akiishi na familia yake.
Pichani (chini na juu) ni baadhi ya Wanajumuiya, wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wakiwa msibani kumpa pole na kumfariji Mwanajumuiya mwenzao usiku wa kuamkia leo.
![]() |
| Mwanajumuiya Seba (mwenye fulana nyeupe) akiwa na Mwenyekiti pamoja na Wanajumuiya wengine baada ya mazishi |
"BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA ... JINA LAKE LIMIDIWE" UPUMZIKE KWA AMANI MPENDWA WETU APOLITO A. RITTE.




No comments:
Post a Comment