JUMUIYA YA MARAFIKI WA KINONDONI
SALAM ZA MWAKA MPYA 2016
Wanajumuiya,
Ni matumaini
ya kila mmoja wetu kwamba mwaka huu 2015 unaisha ukiwa na changamoto na mafanikio yake. Kwa ujumla,
kama Jumuiya mwaka 2015 umekuwa ni mwaka wa mafanikio kwetu tangu tulipoona
hitaji la kuwa Jumuiya na tulipoanza utekelezaji wake kwa mbinu na njia
mbalimbali. Sote tunakumbuka jitihada tulizofanya katika kuhakikisha Jumuiya
yetu inasimama imara na wote tumejitolea kwa hali na mali katika kufanikisha
jambo hilo.
Wanajumuiya,
Ni takriban
miezi mine (4) tu tangu tuirasimishe Jumuiya yetu kwa kuandaa Katiba na baadaye
kufanya uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ambao wanatarajiwa kuhudumia Jumuiya
kwa kipindi cha miaka mitati (3) kuanzia mwezi Septemba, 2015 mpaka Septemba, 2018.
Hadi kufikia tarehe 31 Disemba, 2015, Jumuiya ina jumla ya wanachama 41. Wanachama
hawa wote kwa pamoja wana lengo la kuifanya Jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni
kuwa ni Jumuiya yenye kuwaunganisha pamoja wakati wote na kuwaletea manufaa. Kimsingi
Jumuiy, kama taasisi au mkusnyiko mwingine wowote, ina malengo mbalimbali
ambayo ni ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu kama ifuatavyo: -
1. Malengo ya muda mfupi ((Oktoba 2015 – Machi, 2016)
1.1.
Kusajili
jumuiya katika mamlaka za nchi ili
kuifanya iwe rasmi na itambulike kisheria,
1.2.
Kufungua
akaunti ya benki,
1.3.
Kupanga
ofisi ya Jumuiya,
1.4.
Kuongeza
idadi ya wanachama,
1.5.
Kuendelea
kukusanya michango na ada mbalimbali toka kwa wanachama ili kukuza mifuko
mbalimbali ya Jumuiya.
2. Malengo ya muda wa kati (Machi 2016 – Machi, 2018)
2.1.
Kubaini
fursa mbalimbali za kiuchumi na kimaendeleo kwa Jumuiya,
2.2.
Kuwezesha
upatikanaji wa huduma za bima ya afya kwa wanachama wote,
2.3.
Kuanzisha
na kuingia ubia wa kibiashara kati ya Jumuiya na Wanajumuiya,
2.4.
Kuanzisha
chama cha akiba na mikopo (SACCOS) kwa wanachama na jamii kwa ujumla,
2.5.
Kuongeza
idadi ya wanachama,
2.6.
Kuendelea
kukusanya michango, ada na tozo mbalimbali toka kwa Wanajumuiya
3. Malengo ya muda mrefu (2015 na kuendelea)
3.1.
Kuwekeza
katika miradi ya ardhi, kilimo na ufugaji,
3.2.
Kuchangia
gharama za elimu kwa wanajumuiya wenyewe na watoto/wategemezi wao,
3.3.
Kumiliki
eneo (estate) la Jumuiya litakalokuwa na huduma zote za kijamii kama vile,
nyumba za makazi za wanajumuiya na familia zao, shule, hospitali, soko, maduka madogo
na makubwa, viwanja vya michezo, n.k.
3.4.
Kuingia
ubia na kununua hisa kwenye makampuni mbalimbali,
3.5.
Kuanzisha
viwanda vidogo vidogo na vikubwa,
3.6.
Kufungua
kampuni zitakazojihusisha na biashara mbalimbali,
3.7.
Kuongeza
idadi ya wanachama,
3.8.
Kuendelea
kukusanya michango, ada na tozo mbalimbali toka kwa Wanajumuiya.
Wanajumuiya,
Tukiyasoma na
kuyatafakari haya malengo yote, tunajifunza kwamba hakuna linaloshindikana
iwapo wote tutakuwa na lengo la kutumia vyema fursa vipaji na nafasi tulizonazo
katika kuyatimiza yote. Lakini pia, ni ukweli kwamba bila ya nguvu kubwa ya
kiuchumi inaweza kutugharimu muda mrefu kufikia angalau robo ya malengo hayo. Yatakapotimia
itakuwa ni faida kubwa kwetu sote na vizazi vyetu!
Wanajumuiya,
Mwaka 2016 ni
mwaka wetu wa kuthibitisha kuwa sisi ni Jumuiya ya kutolewa mfano kwa masuala
yote yanayohusu Jumuiya kama yetu au zinazofanana na Jumuiya yetu. Mtaji mkubwa
kabisa tulionao ni huu umoja wetu, kujitoa na kujitolea kwetu na zaidi upendo
na ushirikiano wetu. Kila mmoja akitimiza wajibu wake ipasavyo, hakuna
litkalotushinda huko mbele!
Wanajumuiya,
Kwa niaba ya
viongozi wote wa Jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni, nawatakia heri, baraka, afya
njema na mafanikio tele katika mwaka 2016 na miaka mingine yote ijayo.
Yahya Poli,
Mwenyekiti –
jumuiya ya Marafiki wa Kinondoni,
Wasiliana nasi: -
Twitter: @rafikinondoni
Instagram: rafiki_kinondoni